Viongozi Lamu washutumu mauaji ya afisa wa polisi .
Na Francis Mwaro
Viongozi mbali mbali katika kaunti ya Lamu wamekashifu vikali mauaji ya kinyama dhidi ya afisa wa polisi Hesbon Anunda yalifanyika katika kisiwa cha Pate .
Mauaji hayo ya afisa huyo kwa jina maarufu la Madrasa alipotea alipokuwa ametoka Kizitini akiekea Tsulwa kabla ya kupatina siku nne badaye msituni akiwa ameuwawa kinyama na mwili wake kutupwa huku ukipati na majeraha mabaya ya panga.
Aliyekuwa gavana wa lamu Issa Timammy ameitaka idara ya usalama kufanya uchunguzi wa kina na kuwatia mbaroni wale wote ambao walihusika na mauaji ya afisa huyo.
Kwa upande wake mwakilishi mteule eneo hilo Amina Khalid amesononeshwa na mauaji ya afisa huyo ambaye alipatikana siku nne akiwa amechinjwa kinyama.
Hata hivyo viongozi hao wamekashifu hatua ambao ilichukuliwa na maafisa wa polisi kwa kuwapiga na kuwajeruhi watu zaidi ya 60.