Mipangilio ya mitihani ya kitaifa yakamilika asema magoha.
Na Francis Mwaro
Waziri wa elimu nchini profesa George Magoha amewaonya wazazi dhidi ya kuwatia wasiwasi wanafunzi ambao wanatarajiwa kuikalia mitahani yao wiki mbili zijazo.
Magoha amewataka wazazi kuwawekelea vikwazo ambavyo maranyingi vinawasababisha wafunzi kukumbwa na msongamano wa mawazo na kuwafanya wanfunzi hao kujitoa uhai.
Waziri wa usalama wa ndani dakiri Fred Matingi amesema serikali imeeka mikakati ya kutosha ili kuimariosha usalama humu nchini pamoja na kulinda usalama wakati wa mitihani hiyo ya kitaifa itakapokuwa inaendelea.
Matiangi hata hivyo hakuna afisa wa usalama yeyote ataenda likizo wakati mitihani wakiimiarisha usalama na kulinda mitihani hiyo ya kidato cha nne nay a darasa la nane.
Alizungumza haya wakati wa mkutano uliowaleta pamoja washikadu kutoka wizara ya elimu katika chuo cha mafunzo cha serikali jijini Nairobi.
Wizara zote mbili zile ile ya elimu nay a usalama wa ndani zimeweka mikakati na kutengeneza kituo cha mawasilinano ambacho kitakuwa katika jumba la Harembee jijini Nairobi.