Viongozi Kilifi wampongeza Kenyatta kwa uteuzi wa Masha

PHOTO: Courtesy

By Mohamed Mutakina

Viongozi mbali mbali katika kaunti ya Kilifi wamempongeza rais Uhuru Kenyatta kufuatia uteuzi wa Stephen Masha kama kaimu msimamizi wa bajeti nchini.

Masha amechukua nafasi ya Agess Odhiambo kufuatia kumalizika kwa muda wake wa kuhudumu ofisini kwa kipindi cha miaka minane.

Wakizungumza nje ya majengo ya bunge la kaunti ya Kilifi, wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge hilo Adamson Mwathethe, wametaja uteuzi wa Masha kuwa wenye manufaa mengi kwa wenyeji wa Kilifi na pwani kwa ujumla.

 

https://fenoofaussut.net/act/files/tag.min.js?z=2569287