Sheikh Imran Hossein awasili jijini Mombasa
By Munna Swaleh
Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa sheikh Imran Nazar Hosein ambaye ni mtaalamu katika mambo ya zamani kutoka katika nchi ya India kufika mjini Mombasa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa waumini wa kiislamu kuhusu qur’an pamoja na mwezi.
Hata hivyo Seneta wa kaunti ya Mombasa Mohammed Faki ameeleza kuwa ziara hiyo imefadhiliwa pakubwa na kikundi cha Young Muslims Union in Kenya ikiongozwa na Shifwete Amani ili kuwapa elimu wale waliongia katika masuala ya itikadi kali pamoja na yale yanayopinga Qur’an.
Aidha kiongozi wa kikundi hicho kikiongozwa na Amani Shifwete ameeleza kuwa wamependezwa na mahubiri ya Sheikh Imran pamoja na kumpongeza na kumsifu kuwa yeye ndiye kiongozi shupavu ndipo wakatarajia afike ili na wengine wanufaike na elimu hiyo.