Polisi kwale wachunguza kifo cha mwanafunzi kilichotekea kwenye ufuo wa bahari
Polisi katika eneo la msambweni kaunti ya Kwale weanaendelea kukichunguza kisa ambacho mwanafunzi mmoja wa darasa la nane aliaga dunia kwenye ufuo wa bahari wa Trade Winds huko diani jana jioni.
Kamanda wa polisi katika kaunti hiyo Nehemiah Bitok anasema kwamba marehemu ambaye alikuwa miongoni mwa watahiniwa wa mtihani wa KCPE mwaka huu alizidiwa na mawimbi makali ya bahari kabla ya kuzama na kuaga dunia.
Abdhala Omar mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa mwanafunzi wa shuile ya msingi ya Musurwa alikuwa ameandamana na wanafunzi wenzake kwenye ufuo huo wa bahari.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti ya hospitali ya rufaa katika kaunti hiyo