Kikao cha kamati cha kutatua mzozo wa mgao wa fedha za kaunti chahairishwa
By Mohamed Mutakina
Matatizo ya kifedha yanayoendelea kukumba serikali za kaunti kutokana na mabunge mawili kutafautiana kuhusu mgao wa kaunti wa mwaka huu wa kifedha utaendelea kwa muda .
Kamati ya upatanisho inayojumuisha wabunge wa bunge la kitaifa na Seneti iliyobuniwa kutatua mzozo wa mswada wa ugavi wa serikali za kaunti kwa mara nyingine imebidi kutibuka baada ya wawakilishi kutoka Seneti kususia mkutano huo.
Wakipinga hatua hiyo ya Maseneta ,kiongozi wa wengi bunge la kitaifa Aden Dualle alitaka kikao kuendelea ila maseneta mawili waliokuwa wamefika walitofautiana naye na kulazimu mwenyekiti wa kamati Kimani Ichungwa kuhairisha kikao hadi mwezi ujao.
Kamati hiyo pia imeamua kuwaalika wadau husika wakiwemo baraza la magavana na tume ya ugavi raslimali kujieleza kwenye kikao kitakachofuata.