Kinoti awasili Mombasa kuchuguza ufisadi unaoendelea katika kaunti hiyo

By Zarina Kassim

Hali ya wasiwasi imewakumba baadhi ya Maafisa wa kaunti ya Mombasa baada ya mkuu wa idara ya upelelezi George kinoti kuwasili kwa uchunguzi huku akiapa, kusalia katika kaunti hiyo hadi atakapofanikiwa kuwakabili watu fisadi.

Wachunguzi walioandamana naye tayari wameanza kukagua stakabadhi ya zabuni katika bandari ya mombasa huku baadhi ya mafisa wakitakiwa kuwasilisha tarakilishi zao kwa uchunguzi zaidi.

Miongozi mwa maswala makuu yanayochunguzwa ni kuingiza bidhaa nchini kinyume na sheria na pia mafuta ya kupikia ya zaidi shilingi bilioni 10 yaliyonaswa hivi karibuni.kadhalika kumekuwa na uchunguzi kuhusu wizi wa mafuta ya petroli katika kituo cha kupakia mafuta cha kilindini.

Mafisa wa mamlaka ya ukusanyaji kodi KRA na wa taasisi ya ukadiriaji ubora wa bidhaa KEBS pia watachunguzwa.

 

 

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287