Mauti Barabarani: Watu watatu wafariki dunia katika ajali

Watu watatu wamefariki dunia  usiku wa kuamkia leo kwa kuhusika katika ajali za barabarani katika maeneo tofauti kwenye barabara ya Mombasa-Nairobi .

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi  wa Makueni  Joseph Naimeiyan, mtu wa kwanza mwenye umri wa miaka aroubani na tisa amefariki dunia wakati basi lililokua likitoka upande wa Mombasa kugonga nyuma wa trella lililokua limeegeshwa kando ya barabara kwenye eneo la kibwezi.

Katika ajali ya pili mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na saba amefariki baada ya kugongwa eneo la Machinery na katika ajali ya tatu mwanamume ambaye hajatambuliwa amepatikana katika eneo la Mukaa akiwa amegongwa na gari ambalo halijajulikana kwani lilitoweka.

https://fenoofaussut.net/act/files/tag.min.js?z=2569287