Ufunguzi mpya wa bandari ya Kisumu yahairishwa
By Noah Mwachiro
Shughuli ya kuifungua upya bandari ya Kisumu ambayo iliigharimu serikali kima cha shilingi bilioni tatu iliyotarajiwa kufunguliwa leo baada ya kufanyiwa ukaraabati kwa muda wa miezi minane imehairisha .
Hatua hii inahiri baada ya kamati ya uzinduzi inaongozwa na gavana wa kaunti hiyo Anyang Nyong’o kutangaza kuwa hafla hiyo haitafanyika kama ilivyopangwa.
Rais Uhuru Kenyatta pamoja na kinara wa ODM Raila Odinga walitarajiwa kuwaongoza marais wenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli ,Yoweri Kaguta Museveni na viongozi wengine wa afrika mashariki .
Bandari hiyo inatarajiwa kufufua uchumi wa Kenya kwa kiwango kikubwa pamoja na mataifa jirani ambayo yanapakana na ziwa Victoria.