Naibu gavana wa Lamu awasuta wanaokashifu utendakazi wa NHIF

PHOTO: Courtesy

By Njoki Mwaura

Naibu gavana wa kaunti ya Lamu Abdhulhakim  Aboud amewakashifu viongozi ambao wanaingiza siasa kuhusiana na utendakazi wa kadi za Bima ya NHIF Katika kaunti ya Lamu.

Aboud, ametoa wito kwa wakaazi wa kaunti hiyo kupuuzilia mbali viongozi ambao wanakejeli kupeanwa kwa bima hizo ambazo zitawasaidia wakati wakiwa na wagonjwa katika hospitali husika.

Aidha, Aboud amesema kuwa wakaazi waliojisajili katika mpango huo watapata kadi zao kupitia afisi za wawakilishi wa wadi katika maeneo yao.

Vile vile Aboud amepinga hatua ya viongozi ambao wanataka hafla maalum ya sherehe kwa kupeanwa kwa kadi hizo huku akisema la muhimu ni kuhakikisha wakaazi wanapata kadi hizo ili ziwasaidie kupata matibabu.

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287