Heshimuni sekta ya maboti- Mohamed Somo, msimamizi wa BMU Lamu
By Mohamed Mutakina
Sekta ya maboti katika kaunti ya Lamu inapaswa kuheshimiwa ikizingatiwa kuwa imetoa ajira kwa vijana wengi wa kaunti hiyo.
Msimamizi wa fuo za bahari na maswala ya uvuvi (BMU katika kaunti hiyo, Somo Mohamed Somo amesema kuwa sekta hiyo imekua kitega uchumi katika kaunti hiyo.
Ameongeza kuwa, sekta ya maboti imeajiri takriban vijana 335 hivyo basi akiitaka serikali ya kaunti kuekeza katika sekta hiyo ili kusaidia vijana kukidhi mahitaji ya familia zao.
Aidha amedokeza kuwa vijana wengi katika kaunti hiyo wanajihusisha na uendeshaji wa maboti na kupunguza mambo ya kihalifu kama vile kupiga watu mapanga na hata kuingilia mihadarati.