Viongozi wa pwani washinikizwa kukabiliana na ndoa za mapema

Serikali za kaunti eneo la pwani zimeombwa kushirikiana kwa pamoja kwa kubuni mbinu mwafaka ili kupigana na mimba na ndoa za mapema ambazo zimekithiri.

Mwanzilishi wa shirika la kukabiliana na ndoa za mapema la niache nikomae Karisa Fagio anasema kwamba mimba za mapema zinaathiri pakubwa jamii na pia ndoto za watoto kufifia.

Kwa mujibu wa Fagio takribani wasichana wadogo  elfu 17 huko kaunti ya kilifi wametungwa mimba huku wengine 850 wakiambukizwa virusi vya HIV.

https://fenoofaussut.net/act/files/tag.min.js?z=2569287