Viongozi wazidi kuutilia shaka mswada wa ‘punguza mzigo’

PHOTO: Courtesy

Huku mchakato mzima wa punguza mzigo ukiendelea viongozi mbali mbali wanazidi kuutilia shaka kwamba huenda ni njia moja ya kurudisha waliokuwa mamlakani kujitafutia nafasi za kurudi tena  kwenye viti.

Akiongea na wanahabari aliyekuwa katibu wa serikali ya kaunti ya Mombasa Francis Thoya amesema kuwa hiyo ni njia nzuri lakini nilazima asilimia 25 ya maazimio yao yapigwe msasa.

Thoya amesema kuwa mkenya kwa sasa anaumia sana kimaisha ikilinganishwa na hapo awali.

Aidha amedokeza kuwa serikali kuu na zile za kaunti zinapitia changamoto kubwa na idadi ya wafanyakazi kuhusiana na pesa za kulipa mishahara wafanyakazi wake.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287