Laboso amiminiwa sifa kem kem kwenye ibada ya wafu kwa ajili yake
By Noah Mwachiro
Ibada ya wafu kwa ajili ya aliyekuwa gavana wa Bomet marehemu Joyce Laboso inaendelea katika kanisa la All Saints Cathedral jijini Nairobi. Viongozi mbalimbali wakiongozwa na naibu wa rais William Ruto wamehudhuria ibada hiyo.
Aidha katika baadhi ya hotuba za waombolezaji marehemu Laboso ametajwa kiongozi aliejitolea kwa manufaa ya wenzake.
Laboso ambae amesoma katika shule ya wasichana ya Kenya High ametajwa kuwa alianzaa uongozi akiwa katika shule ya upili, aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule hio mwaka 1979 wakati marehemu Laboso alikua kidato cha nne Margret Wanjohi, alisema Laboso alikua kielelezo kwa wanafunzi wenzake.
Kwa upande wake mkewe kiongozi wa ODM Raila Odinga, Idah Odinga ambae pia alikua mwalimu wa Laboso katika shule ya Kenya High, amemtaja marehemu kuwa alionyesha mfano bora unaostahili kuigwa na viongzi wengine haswa wale wa kike.
Amesema Kenya imepoteza kiongozi huku akiwapa changamoto viongozi walioko katika nyadhifa mbalimbali, kuhakikisha kwamba wanaeka mikakati kukabili ugonjwa wa saratani unaondelea kuangamiza wakenya wengi.
Laboso amemuacha mjane Edwin Abonyo na wanawe wawili, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 juma lililopita kufuatia saratani.
Kwengineko mwili wa aliyekua mbunge wa kibra ken okoth umewasilishwa katika shule ya Moi mtaani Kibra ambapo ibada nyengine ya wafu kwa ajili yake inaendelea .