Wanabodaboda watakiwa kudumisha nidhamu na usafi Kilifi
Wahudumu wa bodaboda katika vituo vyote kaunti ya kilifi wametakiwa kudumisha nidhamu na usafi kwa wateja wao .
Wito huu umetolewa kwa wahudumu wa bodaboda eneo la Majengo Kanamai eneo bunge la Kilifi kusini na Kenya nzima kwa jumla kuzingatia nidhamu katika utendakazi wao.
Wahudumu hao wamehimizwa kuonyesha nidhamu kwa wateja wao hasa wanapofika maeneo ya kuegesha pikipiki almaarufu leba kwa kutumia lugha zinazostahili kwa wateja wao,.
Mwakilishi wa wadi ya Mtopeni Victor Mwagandi amewataka wahudumu hao kudumisha usafi kwa lugha zinazostahili kwa wateja wao kutokana na kutangamana na watu wengi katika utendakazi wao wa kila siku.
Kulingana na mwakilishi wa wanawake kaunti hiyo Getrude Mbeyu wakati umefika kwa wahudumu hawa kuonyesha mfano mwema na kuipelekea jamii kubadili dhana mbaya waliyonayo dhidi ya wahudumu wa bodaboda.