Wafanyabiashara wakanusha madai yakuchafua mazingira Mombasa
By Mohamed Mutakina
Muungano wa wafanyabiashara wadogo kaunti ya Mombasa wamekanusha madai kuwa wanachama wake wanachangia pakubwa uchafuzi wa mazingira.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Hamis Dawa, amedai kwamba serekali ya kaunti imezembea katika kudumisha usafi wa jiji la Mombasa.
Wakati huo huo wafanyabiashara hao wamelalamikia kuhangaishwa na maafisa wa kaunti ya Mombasa.