Fanyeni uchunguzi ndio mushike washukiwa wa ufisadi- Lonyangapua, Gavana Pokot
Gavana wa Pokot magharibi Proffesa John Lonyangapua amesema kwamba anaghadhabishwa na jinsi ambavyo washukiwa wa ufisadi wanavyokamatwa ovyo ovyo hata kabla ya uchunguzi kufanywa kuhusu suala zima .
Amesema mshukiwa yeyote waufisadi anafaa kuheshimiwa hadi wakati ambapo Mahakama itadihirisha iwapo amehusika au la. Kauli yake inajiri wakati ambapo viongozi kadhaa akiwemo gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu amekamatwa na kuzuiliwa kufuatia ufisadi.
Waititu aliachiliwa jana na mahakama na anatarajiwa kuondoka katika gereza la Industrial Areas hii leo baada ya kulipa dhamana ya shilingi million 15 pesa taslim.
Gavana huyo pamoja na mkewe Susan Wangari walilazimika kulala korokoroni baadaa ya kukosa kulipia dhamana hio hapo jana