Elimu ya dini ni muhimu kwa taifa- Mohamed Faki, Seneta wa Mombasa
Kama njia mojawapo ya kuwaepusha watoto wa kiislam na ugaidi na itikadi kali, Seneta wa Mombasa amesema kuna haja ya kuwapa elimu nzuri ya madrassa ili kuwafunza kufuata njia za mwenyezi Mungu.
Akiongea na wanahabari kwenye hafla ya watoto wa Masjid Sunnah seneta wa kaunti ya Mombasa Mohammed Faki amesema kuwa taifa bila elimu ya dini huwa na visa vinavyotatiza amani ya nchi.
Aidha Faki, amewataka viongozi kuja na mpango wa elimu nadharia katika vyuo vya kidini ili kuweza kuwapa watoto elimu zote bila upendeleo wowote.
Wakati huo huo ameutaka uongozi wa msikiti huo kuja na mpango wa kufungua vyuo vya elimu nadharia na kuacha kutegemea karo kutoka kwa madrassa peke yake ili kuweza kukuza elimu za madrassa.
Hata hivyo amesema kuwa mpango huo utawezesha kupata fedha za kusimamia walimu na majengo yaliyopo.