Tunataka soko, zahanati na shule- Wakaazi wa Ganda, Malindi
By Mohammed Ali
Wakazi wa kijiji cha Sokomoko wadi ya Ganda huko Malindi wamesema wana uhitaji wa soko, zahanati na shule.
Mary Kidatha, mkaazi wa eneo hilo amesema imekuwa vigumu kupata mahitaji yao wakidai uongozi wa hapo awali haukuzingatia masuala muhimu ya maendeleo mashinani.
Vile vile Faustina Mwamuye, ameelezea kufurahishwa na hatua ya kutolewa kwa tarehe mpya ya uchaguzi mdogo na tume ya IEBC eneo hilo, wakidai kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta miradi muhimu bila mafanikio kwa kukosa kiongozi.
Kadhalika, amesema kumeshuhudiwa utata katika ugavi wa fedha za basari kwa wanafunzi na kuongeza kwamba kuna haja ya kuchagua mtu binafsi wala sio kuangalia chama.
Uchaguzi mdogo wa Ganda utafanyika tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka huu.