Wakaazi wa Voi waishtumu serikali ya kaunti kwa kuwatoza ushuru mara mbili
By Zarina Kassim
Muungano wa wafanyibiashara wa vichinjio mjini Voi katika kaunti ya Taita Taveta wameikosoa vikali serikali ya kaunti hiyo kwa kuwatoza ushuru mara mbili.
Wafanyibiashara hao wanadai kuwa wamekuwa wakitozwa ada kwa kila mnyama wanaemchinja licha ya kuwa wamelipa liseni ya kuendesha biashara hiyo.
Vile vile wanadai kuwa serikali hiyo bado haijatilia maanani mapendekezo yaliyotolewa kwa wananchi kuhusiana na ada ambayo wanatozwa ili kuendesha biashara hiyo.