Kenyatta asisitiza serikali kuu haina pesa ya ziada kuwapa magavana
Rais Uhuru Kenyatta amewataka magavana na maseneta kuweka wazi malengo yao ya kuitisha fedha zaidi kwa serikali za kaunti, akisema kuwa serikali ya kitaifa haiwezi kutoa fedha zaidi kwa serikali hizo.
Aidha, Kenyatta amesema kuwa hana fedha za kutosha kuwapa serikali za kaunti huku akiwahimiza wagavana hao kubuni mbinu za kusimamia shughuli za ugatuzi, kulingana na fedha walizotengewa.
Rais aliyasema hayo wakati alipohudhuria mazishi ya Raham Wambui ambaye ni mama wa Peter Kenneth.
Kwa upande wake naibu wa rais daktari William Ruto, amesema kuwa serikali itaendelea kuwafanyia maendeleo wakenya huku akisistiza kuwa huu ni wakati wa wakenya kujitenga na siasa za kikabila.