Joho afanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri

PHOTO: Courtesy

PHOTO: Courtesy

By Mohamed Mutakina

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri, ambapo maafisa wakuu 16 wa idara mbalimbali wameathirika na mabadiliko hayo.

Afisa mkuu wa  idara ya biashara na uwekezaji katika kaunti hii Abdulwahab  Mbarak,  amehamishwa katika idara ya maji na rasilimali asili huku Josphita Mwajuma, akihamishwa hadi katika idara ya ardhi.

Katika mabadiliko hayo, Francis Kombe atashikilia idara ya mazingira huku Tuli Mwalukumbi ambaye alikuwa kwenye idara ya elimu, akihamishwa hadi kwenye idara ya biashara na uwekezaji.

Afisa mkuu wa afya ya umma Aisha Abubakar na mwenzake wa huduma za matibabu daktari Khadija Shikeli wakisalia katika idara zao huku mabadiliko zaidi yakitarajiwa kufanywa.

Kaimu katibu wa serikali ya Mombasa Joab Tumbo, amesema kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuboresha huduma kwa wakaazi wa mombasa.

https://pertawee.net/act/files/tag.min.js?z=2569287