Wakaazi wa Lamu walilia hifadhi ya maiti ya kisasa

PHOTO: Courtesy

PHOTO: Courtesy

By Mohamed Mutakina

Serikali ya kaunti ya Lamu kupitia idara ya afya imetakiwa kujenga hifadhi ya maiti yenye muundo wa kisasa katika hospitali kuu ya kaunti hiyo ya King Fahad.

Naibu mwenyekiti wa jamii ya Wameru kaunti ya Lamu Silas Kimathi, amesema kuwa jamii ya wakristo wanaoshi katika  mji wa Lamu wanakumbwa na changamoto kwa kukosa mahali pa kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo na kulazimika kuwasafirisha hadi Mpeketoni ambapo ni gharama ya juu.

Aidha, Kimathi amesema kuwa chumba kinachotumiwa kama hifadhi ya maiti katika hospitali ya King Fahad, kwa sasa kiko katika hali mbaya kwani hakina vifaa hitajika kwa shughuli za kuhifadhia maiti.

Kauli yake imeungwa mkono na mshirikishi wa shirika la Haki Afrika katika kaunti ya Lamu, Yunus Ishaq ambaye amesema ipo haja ya hospitali hiyo kufanya hivyo ili iweze kuhudumia wale wenye itikadi ya kuhifadhi maiti zao kabla ya kuwazika.

Ishaq, amesema kaunti ya Lamu iko na watu wenye dini tofauti tofauti, hivyo basi ni haki ya kila mwananchi wa Lamu kuhudumiwa kikamilifu bila kujali misingi ya kidini.

https://pertawee.net/act/files/tag.min.js?z=2569287