Hati miliki 70 zafutiliwa mbali na serikali Kuu katika kaunti ya Kwale
By Noah Mwachiro
Serikali imefutilia mbali jumla ya hati miliki 70 za ardhi yenye utata katika eneo la Maji ya Chumvi, kinango katika kaunti ya Kwale
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya pwani John Elungata amesema kuwa hati miliki hizo zilikuwa na dosari akiagiza hati miliki zilizo sahihi kukabidhiwa kwa wamiliki wa ardhi hizo kabla ya mwezi huu wa julai kumalizika
AKizungumza katika eneo la mji wa chumvi Elungata ameionya kamati iliyoongoza zoezi la kupima ardhi hio na kuwakabidhi watu wengine kuzirudisha mara moja kwa wenyewe.
Kwa upande wake waziri wa ardhi katika kaunti hiyo Saumu Baya amesema kuwa ardhi hiyo ilifaa kupimiwa wakaazi wa eneo hilo na wala si wanyakuzi wa ardhi.