Polisi wakana kuhangaisha wakaazi Kisauni
By Nuria Omar
Maafisa wa usalama katika eneo la Kisauini kaunti ya Mombasa wamejitenga na shutma wanazoelekezewa kuwa wamekuwa wakiwahangaisha wakaazi hususan vijana katika eneo hilo wakati wa usiku.
Naibu kamishana wa eneo hilo Kipchumba Ruto amesema kuwa maafisa wa polisi hawakuhusika kivyovyote na visa hivyo akiitaka afisi ya upelelezi katika eneo hilo kufanya uchunguzi kuhusiana na madai hayo.
Vile vile ameitaka jamii kushirikiana na idara ya usalama ili kuyamaliza magenge ya kihalifu ambayo yanawahangaisha waakaazi katika eneo hilo.