WABUNGE WA KIKE WATAKIWA KUANDAMANA NJE YA BUNGE.

Mbunge wa Kibera Ken Okoth amewataka wabunge wa kike kufanya maandamano ya amani iwapo bunge halitapitisha mswada wa usawa wa kijinsia ifikapo siku ya Alhamisi wiki ijayo.

Hii inajiri siku moja tu baada ya bunge kushindwa kufikisha idadi inayohitajika ili kuweza kupitisha mswada huo.

Okoth amesema kuwa bunge la kitaifa tayari imeonyesha nia ya kutopitisha mswada huo huku akiwataka wanawake kuamka na kupigania haki zao za kikatiba.

Hapo jana wabunge 195 ndio waliopigia kura mswada huo, wabunge 25 wakipinga huku wabunge 19 wakidinda kupiga kura zao.

KEN OKOTHMswada huo utaregeshwa tena bungeni siku ya Alhamisi wiki ijayo.