MAFUNZO YA NIDHAMU NJEMA KWA MAAFISA WA KAUNTI YA MOMBASA
Huenda ikawa afueni kwa baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Mombasa baada ya shirika la kutetea haki za kibnadam MUHURI kuanzisha mafunzo kwa askari wa kaunti hiyo.
Mafunzo hayo yanapania kubadilisha taswira ya maafisa hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijulikana kukiuka haki za kibinadam.
Kulingana na afisa wa mipangoPeter Shambe wa shirika hilo na amesema lilichukua hatua hiyo baada ya kupokea lawama kutoka kwa baadhi ya wakaazi wa kisauni, kongowea na marikiti kuwa maafisa hao huwanyanyasa.
Shambe amesema ana imani kuwa maaafisa hao watabadili mienendo yao ya kukabiliana na wakaazi.
Hata hivyo amewaomba viongozi kushirikiana ili kumaliza janga la mihadarati ambalo limekuwa donda sugu pwani.