Jopo linalomchunguza Tonuilahairisha vikao vyake hadi wiki ijayo

Vikao vya jopo linalochunguza madai ya ufisadi dhidi ya jaji wa mahakama ya juu zaidi nchini Philip Tunoi vimehairishwa hadi siku ya Jumanne wiki ijayo.
Kupitia wakili wake Pual Linon,Tunoi ameliomba jopo hilo kuahirisha vikao hivyo leo kwa kuwa,kesi aliyowasilisha akipinga kustaafu akiwa na umri wa miaka sabini inaendelea leo.
Kwa upande wake Tunoi amesema kuna haja ya kesi ya umri wake ihairishwe ili jopo lililoteuliwa na rais litekeleze uchunguzi wake kikamilifu.
Hatahivyo mwenyekiti wa jopo hilo Sharad Rao amemhakikishia jaji huyo vikao vya haki na kumtakia kilalakheri.