Djokovic atwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Miami

Bingwa wa mchezo wa tenisi duniani kwa wanaume Novack Djokovic ameendelea kutamba kwa kutwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Miami.
Djokovic ametwaa ubingwa huo kwa kumshinda mpinzani wake Kei Nishikori, kwa kumchapa kwa jumla ya seti mbili za 6-3, 6-3.
Ushindi huo unampa nyota huyu wa tenisi taji la 63 toka alivyoanza kucheza mchezo huo.
Kutokana na ushindi huo Djokovic anakuwa miongoni mwa wacheza tenesi wanaoingiza pesa nyingi na akiwa amefikisha kiasi cha pauni milioni 100, katika muda aliocheza mchezo huo.