Vijana wa Kenya U-20 waanza vyema michuano ya Afrika

 

Timu ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20 wamefanikiwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Sudan  kwa mchezo wa raundi ya kwanza katika michuano ya kufuzu kwa kombe la bara la Afrika kwa vijana.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo vijana wa Sudan walikuwa kifua mbele katika mchezo huo baada ya kupachika bao la kwanza,huku Kenya  ikisawazisha  katika  kipindi cha pili kupitia mkwaju wa mchezaji wa Gor Mahia Amos Nondi.

Haya ni matokea mazuri kwa vijana hao wa nyumbani kwani imewapa nafasi ya kuingia  raundi ya pili ya michuano hiyo.