Starlets kuelekea Algeria kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la Afrika

Timu ya taifa ya wanadada nchini Starlets wataondoka nchini hapo kesho kuelekea Algeria kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la bara la Afrika.
Starlets watajimwaya ugani kuchuana na Algeria wakiwa nyumbani kwao kwa mchezo wa raundi ya kwanza katika ngarambe hizo itakayotimua kivumbi siku ya Ijumaa.
Kikosi hicho cha vidosho 20 kikokambini katika uwanja wa kasarani.
Iwapo Starlets watawachapa wanadada wa Algeria basi watakuwa na uwezo mkubwa wakuingia katika michuano hiyo itakayoandaliwa nchini Cameroon mwaka huu kati ya tarehe 19 November hadi hadi 3 December
Kikosi hicho kinaongozwa na mkufunzi mkuu David Ouma, naibu wake Mary Adhiambo na mkufunzi wa walindalango Lawrence Webo