Toure kuondoka Man City

 

Nyota kiungo kati wa klabu ya Manchester City,Yaya Toure ataihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Haya ni kwa mujibu wa wakala wake Dimitri Seluk kusema kuwa klabu hiyo iliyoko katikati mwa jiji la Manchester haiko tayari  kumpa Toure mkataba mpya.

Hatahivyo Seluk ameishutumu Man City kwa kumuonyesha dharau Toure kwa kujivuta kumpa mkataba mpya.

Kufikia sasa kiungo huyo wa kati Yaya toure anahusishwa kujiunga na klabu ya PSG, Bayern Munich na  Juventus.