MCK yawaonya wanahabari wanaoenda kinyume na maadili
Baraza la waandishi wa habari nchini MCK limetoa onyo kwa waandishi wa habari wanaojihusisha na visa vinavyokwenda kinyume na maadili ya uandishi wa habari.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari ,afisa mkuu mtendaji wa baraza hilo Dakta Haron Mwangi amesema kuwa MCK imekuwa ikipokea taarifa za visa vya ufisadi miongoni mwa waandishi wa habari, na kusema kuwa yeyote atakayepatikana na kosa hilo atapokonywa stakabadhi za kutekeleza majukumu yake.
Aidha baraza hilo limetishia kutaka hadharani majina ya waandishi wa habari ambao wameripotiwa kuhusika katika visa ambavyo haviambatani na kanuni za baraza hilo.
Mwangi amesema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiitisha hongo katika kutekeleza majukumu yao huku wakitumia vitambulishio vya uandishi wa habari kinyume cha sheria.