Simba watundu watoroka tena

Hali ya taharuki yatanda tena kufuatia Simba wengine wawili kuonekana hii leo katika eneo la Kitengela siku moja tu baada ya mwengine kuuawa hapo jana katika eneo la Isinya baada ya kumjeruhi mwanamume mmoja.
Wakazi wa eneo la Nairobi wameonekana kukumbwa na athari zaidi za simba hao ambao wanaonekana kutatiza usalama wa wakazi hao.
Picha za simba hao kutoka kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kuwa simba hao wanatembea kilomita chache kutoka kwenye mbuga ya wanyama.
Hata hivyo maafisa wa KWS wamepeleka ndege kuondoa simba hao ili kuelekezwa katika mbuga ya wanyama kabla majanga zaidi hayajatokea.