Uhuru atoa hotuba ya hatua ambazo serikali yake imepiga

 

Rais Uhuru Kenyatta amelihutubia taifa katika majengo ya bunge kuhusu hatua ambazo serikali imepiga tangu kuchukua hatamu za uongozi mwaka 2013.

Rais amesema kuwa wakenya wanatabasamu kutokana na kuimarishwa kwa huduma za umeme baada ya serikali kwa ushirikiano na washikadau kadhaa kuanzisha miradi miwili mikuu ya uzalishaji wa umeme nchini.

Kuhusu swala la elimu rais amesema kuwa ahadi ambayo waliahidi ya tarakilishi kwa wanafunzi wa darasa la kwanza itatekelezwa mwaka huu.

Kuhusu usafiri rais amesema kuwa serikali imepiga hatua kuhakikisha inaendelea kuunda barabara mpya na hata kukarabati zengine huku akisema kuwa reli ya kisasa itakaminilika mwezi Juni mwaka ujao.

Aidha wabunge wameonekana kuunga rais mkono baada ya kuonyesha kutoridhishwa na jinsi serikali za ugatuzi zinavyojikokota kutekeleza miradi mashinani.

Awali baadhi ya wabunge wa CORD walitatiza hotuba ya rais lakini spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi akaagiza kufurushwa kwa wabunge hao.