Upinzani wakatisha hotuba ya rais bungeni

 

Wabunge na Maseneta wa muungano wa upinzani CORD wamekatisha hotuba ya rais Uhuru Kenyatta katika bunge la kitaifa.

Juhudi za spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi kujaribu kutuliza wabunge wa CORD ziligonga mwamba na hivyo basi kulazimu kuwafurusha wabunge walioaminika kuwa wasumbufu.

Awali kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale alidai kuwa muungano wa CORD una njama ya kuzima hotuba ya rais.

Rais Uhuru Kenyatta anafaa kuhutubia taifa kuhusu hatua zilizopigwa na serikali ya Jubilee baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwaka 2013.