Uhaba wa madaktari wa afya ya akili waikumba Kenya

Kenya inakumbwa na uhaba wa madakatari na wahumudu wa afya ya akili huku kukiwa na madakatari 120 na wahudumu 420 kote nchi huku wengi wao wakijihusisha na tiba ya kibinafsi hali inayowashinda waathiriwa wengi kupata mataibabu.
Akiongea katika warsha ya washikadau wanaoshughulikia swala la afya ya akili mtafiti Ireri Mugambi amesema kuwa serikali imelifungia macho swala la afya ya akili huku kukiwa hakuna utafiti wowote uliofanywa na wizara ya afya kutambua hali halisi na idadi ya watu walioathirika huku taasisi zilizo na taarifa zikikataa kutowa taarifa hizo.
Ireri amesema kuwa ipo haja kwa wizara ya afya kuboresha kanuni zake na kuangazia maswala ya afya ya akili kwani una athiri watu wengi huku ikiongeza unyanyapaa katika jamii kwa kukosa vituo tiba ya akili mashinani.