Taarifa kutoka mahakama kuu ya Mombasa

Msichana wa umri wa miaka 17 anayetuhumiwa kwa kosa la wizi kwa njia ya udanganyifu katika eneo la Tudor Kaunti ya Mombasa amefikishwa mahakamani na kukubali kosa hilo.
Mshtakiwa Mary Wanjiru ameiambia mahakama kuwa hakufanya kosa hilo kwa kukusudia ila alitumwa kufanya kitendi hicho na mtu ambaye alikuwa akimpa hifadhi katika nyumba yake.
Hakimu mkuu Susan Shitubi amesema kuwa lazima mshtakiwa huyo afanyiwe uchunguzi wa umri wake kabla ya kutoa hukumu dhidi yake tarehe 7 mwezi ujao ,wakati kesi hiyo itakapo amuliwa.
Shtaka dhidi yake ni kuwa mnamo tarehe 20 mwezi uliopita mshtakiwa huyo alimtilia dawa za kulevya Kelvin Gathenya na kumuibia mali yenye thamani ya shilingi laki moja na elfu 10.