Kariobangi Sharks kukaza buti katika michuano iliyosalia

 

Mkufunzi wa Kariobangi Sharks,Mike Amanga amesema kushindwa kwao dhidi ya KCB wikendi iliyopita kumetoa mwelekeo mpya kwa klabu chake.

 Akizungumza baada ya klabu chake kuzabwa mabao mawili kwa moja, Amanga alikubali kuwa vijana wake walikosea tangia walipocheza na vilabu vingine katika michuano ya Kenya Premier League.

 Amanga aidha amesema makosa hayo yalitokana na wengi wa wachezaji wake kuwa nje kutokana na majeraha huku akisema kuwa hilo halitawatia wasiwasi kwani watazidi kujitahidi kwenye michuano iliyosalia.