Mwafungo atumaini kuwa vijana wake watashinda katika michuano

Mwenyekiti wa muungano wa michezo ya shule tawi la Pwani ,Rodgers Mwafungo amesema kuwa wanaimani na timu zilizofaulu katika awamu ya kitaifa kutoka mkoa wa pwani kuwa zitafanya vyema.
Mwafungo amesema kuwa kikosi chake kinachojumuisha shule ya upili ya Agha khan ya wanaume na Kaya tiwi wanawake upande wa mpira wa kikapu,St Chalse Lwanga Boys na st Johns wanawake kwa upande wa mchezo wa magongo ,na St Geoges kwa upande wa raga 7 kila upande kuwa viko imara kwa sasa kuminyana katika awamu hiyo.
Michezo hiyo ya shule za upili kwa muhula wa kwanza inatarajiwa kuingia katika awamu ya kitaifa tarehe 10-16 Aprili katika shule ya Kamusinga kaunti ya Bungoma.