Arsenal yawafunza soka watoto wakimbizi wa Iraq

Klabu ya Arsenal inashirikiana na shirika la Save the Children kuwajengea viwanja watoto wanaotoroka vita nchini Iraq katika kambi za watu wasio na makao.
Arsenal ina matumaini kuwa mradi huo utawasaidia watoto walio katika hali mbaya kuona furaha inayosababishwa na soka.
Mpango huo unawalenga wavulana na wasichana na kuwahamasisha watoto kuanzisha timu zisizoleta migawanyiko ya kihistoria.