Jopo laundwa kuangalia upya matokeo ya KCSE 2015

 

Wanafunzi zaidi ya elfu tano waliokalia mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka 2015 na matokeo yao kufutiliwa mbali wamepata afueni baada ya kubuniwa kwa timu maalum kuangalia upya matokeo ya wanafunzi hao.

Katika mkutano na kamati ya bunge ya maswala ya elimu uliodumu masaa manne ,waziri wa elimu dkt Fred Matiangi,amethibitisha kuwa tayari jopo hilo limeundwa ili kusikiza kilio cha wanafunzi walioathiriwa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Sabina Chege ameelezea kamati imeridhishwa na hatua hiyo kuwa wanafunzi hao wana haki pia kukataa rufaa iwapo hawataridhishwa na maamuzi ya timu hiyo.

Hata hivyo,wabunge wakiwemo Chris Wamalwa,Ababu Namwamba na Peter Kaluma wanahisi hatua hiyo haitendi haki badala wanataka matokeo yote ya mwaka 2015 kufutiliwa mbali kwa msingi kwamba haukafanyika kwa mazingira wazi na yenye haki.