Ustadh akana madai ya ulawiti Malindi

 

Mwalimu mmoja wa Madrassa katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi amekanusha madai kwamba alimlawiti mwanawe wa kambo.

Mwalimu huyo ambaye alitandikwa na vijana waliokuwa na hasira ameyataja madai hayo kuwa yasio ya kweli yanayolenga kumuharibia jina.

Aidha mama aliyeshuhudia mwalimu huyo akitandikwa amewalaumu vijana hao kwa kuchukua hatua bila kudhibitisha madai yake.

Visa vya ulawiti vimekithiri katika eneo la Malindi huku wazazi wakiomba serikali iwachukilie sheria kali wahusika.