Usafiri watatizika kufuatia msongamano wa magari

 

Shughuli za usafiri wa masafa marefu kutoka jijini Mombasa zimelazimika kucheleweshwa kufuatia msongamano wa magari katika barabara kuu ya Mombasa-Nairobi kufuatia likizo ndefu iliyoanza leo.

Hata hivyo kwa upande wa abiria wamelalamikia kuongezwa kwa nauli maradufu jambo linalowalazimu kukata tiketi siku mbili kabla ya usafiri ili kuepuka msongamano katika kituo cha basi.

Hali hii imetatiza usafiri kwa kiasi kikubwa na kuwaacha abiria katika njia panda wasijue la kufanya zaidi kusubiria mpaka hali itakapokuwa shuwari.