Mshukiwa wa Al Shabab akamatwa Namanga

Mshukiwa mmoja wa Al Shabab anazuiliwa katika kituo cha polisi kaunti ya Kajiado baada ya kunaswa hapo jana katika kizuizi cha polisi eneo la Namanga.
Inadaiwa mshukiwa huyo Baluku Swaleh mwenye umri wa miaka 49 raia wa Uganda alikamatwa jana jioni akiwa anaelekea nchini Tanzania.
Mkuu wa idara ya upelelezi kaunti ya Kajiado Ngatia Iregi alikua akitoka jijini Nairobi kabla ya kuabiri gari la umma huko Namanga ambapo alipatikana na mkoba uliokua na picha za kuonyesha jinsi walivyokua wanatekeleza mashambulizi nchini Somalia,bendera za Al Shabab miongoni mwa vitu vingine.
Aidha imebainika kuwa mshukiwa huyo tayari amekiri kuwa mwanachama wa Al Shabab akisema alijiunga na kundi hilo mwaka 2011 akiwa nchini Somalia ambapo alikua anahudumu kama mwanajeshi wa kikosi cha AMISOM kutoka Uganda.
Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinett amewataka wananchi kuwa wangalifu zaidi wakati huu wa sherehe za Pasaka.
Katika ujumbe wake,Boinett amewataka wananchi wanaoelekea katika maeneo ya ibada,burudani na wanaosafiri kuripoti kisa chochote kisicho cha kawaida ili hatua za haraka kuchukuliwa.
Akitoa mfano wa shambulizi lililotokea jijini Brussels nchini Ubeligiji wiki hii,Boinett amesema ipo bhaja ya wakenya kushirikiana na idara ya polisi katika kudumisha usalama.
Hata hivyo amewahakikishia wakenya kuwa usalama umeimarishwa kila kona ya taifa na kwamba wasiwe na hof ya kuendesha shuguli zao za kawaida.