Dado akana kupelekwa kwa jamii ya wafugaji kujisajili kama wapiga kura Tana River

 

Gavana wa kaunti ya Tana River Hussein Dado amepuzilia mbali madai kuwa jamii ya wafugaji wamepelekwa kujisajili kama wapiga kura wa kaunti ya Tana River na kuonya vikali kuwa madai hayo ni ya uongo ili kugeuza usikivu.

Gavana huyo amesema kaunti hiyo imekuwa ikiongoza kwa idadi ya usajili wa wapiga kura kwa asilimia 50 kutokana na wafugaji waliondolewa makazi yao tangu mwaka 2012 kurudi katika kaunti hiyo.

Haya yanajiri baada ya madai kuibuka kuwa wapiga kura kutoka jamii moja walipewa hongo kukubali kujisajili katika kaunti hiyo ili kushiriki kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Aidha Dado ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuongeza muda wa kuandikisha wapiga kura kuongezwa ili kutoa nafasi kwa mwananchi ambaye hajajisajili au kuchukua kitambulisho kupata nafasi kujisajili kama wapiga kura.