Siku ya kimataifa ya kifua kikuu yaadhimishwa leo

Kenya imeungana na mataifa mengine katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kifua kikuu yani (TB).
Katibu wa kudumu katika wizara ya afya Nicholas Muraguri amesema Kenya imefikisha malengo ya shirika la afya ulimwenguni WHO katika kudhibiti ugonjwa huo.
Hata hivyo Muraguri amedokeza kuwa changamoto katika kupambana na ugonjwa huo ni TB sugu ambayo ni ngumu kutibu.
Wakati huo huo kaunti ya Nairobi iliandikisha asilimia 15 ya visa vya ugonjwa wa TB nchini.
Naibu gavana wa kaunti ya Nairobi Jonathan Mweke amesema kuwa licha ya idadi kubwa ya visa hivyo serikali ya Nairobi imeweka mikakati ya kupunguza ugonjwa huo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ukiwa ni Mulika TB, Maliza TB.