Waiguru akana kufahamishwa kuhusu ufujaji wa pesa za vijana

 

Aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru amekana madai ya kuhusika katika sakata ya ufujaji wa milioni 180 za maendeleo ya vijana akisema kuwa katibu mkuu Peter Mangiti hakumfahamisha.

Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu uwekezaji, Waiguru pia amekana kuwa afisi ya ukaguzi wa mashirika ya umma haukumjulisha kuhusiana na sakata hiyo.

Waiguru aidha amesema kuwa Mangiti ndiye aliyepaswa kufauatilia namna fedha za hazina ya maendeleo ya vijana zilivyotumika huku akisema alifahamishwa pindi tu ufujaji wa fedha hizo ulipobainika.

Hata hivyo ameeleza kuwa hangeweza kuchukua hatua yoyote kwani hakukuwa na ushahidi kuhusiana na sakata hiyo.