KNEC yavunjiliwa mbali kufuatia wizi wa mitihani

 

Maafisa wakuu wa baraza la mitihani nchini,KNEC watashtakiwa kwa visa vya wizi wa mitihani ya kitaifa mwaka uliopita baada ya bodi hiyo kuvunjiliwa mbali hii leo.

Waziri wa elimu Fred Matiang’i amesema uchunguzi umeonyesha wanachama wa bodi hiyo walihusika katika visa kadhaa vya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa ya darasala la nane KCPE na kidato cha nne KCSE mwaka jana mtawalia.

Maafisa hao wakiwemo afisa mkuu wa KNEC Joseph Kivilu,naibu wake Ambia Noor,Thomas McKenzi na wengine watakamatwa mara moja iwapo hawatajisalimisha kwa idara ya usalama.

Rais Uhuru Kenyatta amemteua aliyekua naibu chansela wa chuo kikuu cha Nairobi prof.George Magoha kama mwenyekiti wa bodi hiyo.