Dereva mwengine wa Uber anusurika kifo

Dereva mwengine wa kampuni ya taxi ya Uber amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na kundi la wahalifu na gari lake kuchomwa katika eneo la Riruta viungani mwa jiji la Nairobi.
Dereva wa gari hilo amesema alikuwa akielekea Yaya Center kumchukua mteja wake, kabla ya genge la watu wanne walioshirikiana na mteja wake kumvamia na kuchoma gari lake.
Afisa mkuu wa kitengo cha ujasusi jijini humo Ireri Kamwende amesema wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo, ambalo linajiri mwezi mmoja baada ya dereva mwengine wa ubber kuchomwa katika eneo la Kilimani.